Tuesday, April 17, 2012
MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA BAYERN NA REAL LEO
![]() |
Robben wa Bayern |
![]() |
Ronaldo wa Real |
Bastian Schweinsteiger amerejea baad aya kutumikia adhabu ya mechi moja, lakini Jupp Heynckes amesema jana kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba hana uhakika kama Nahodha huyo Msaidizi ataanza kwa sababu alikosa mazoezi ya kujiandaa na mechi hiyo.
Toni Kroos anaweza kuwapo, wakati Luiz Gustavo anaweza kucheza kama kiungo wa pili wa ulinzi.
Mabeki Daniel Van Buyten anayeumwa mguu na Breno (goti) wote watakuwa nje.
Kocha wa Madrid, Jose Mourinho anatarajiwa kuwaanzisha pamoja Karim Benzema na Angel Di Maria baada ya wawili hao kukaa benchi Jumamosi timu yake ikishinda dhidi ya Sporting Gijon.
Xabi Alonso amerejea baada ya kumaliza adhabu, lakini Ricardo Carvalho na Lassana Diarra wote bado majeruhi na hawatacheza.
JE WAJUA?
•Bayern Munich imeshinda mechi sikta mfululizo za Ligi ya Mabingwa nyumbani na imeshinda mechi 12 kati ya 13 za Ulaya Allianz Arena.•The Bavarian haijawahi kufungwa na na Real Madrid nyumbani (imeshinda nane na kutoa sare moja). Rekodi ya jumla ya Munich dhidi ya Madrid ni kushinda mechi 10, sare 2, kufungwa 6.
•Klabu hizo awali zimekutana katika Nusu Fainali nne, huku Bayern ikishinda mara tatu (1976, 1987 na 2001) na Madrid moja tu mwaka 2000.
•Jupp Heynckes, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa mchezaji wakiitoa Madrid msimu wa 1997-98, hajawahi kuifunga timu ya Hispania katika mechin mbili tangu awe kocha.
•Rekodi ya Real Madrid kutofungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu na ikiwa imefungwa mabao sita tu, inawafanya wawe timu yenye ukuta bora zaidi katika timu zote zilizosalia kwenye michuano hii.
•The Castilian wameshinda mechi moja tu katika ardhi ya Ujerumani katika mechi 22 (Kushinda 1, sare6, kufungwa 15) – ushindi pekee ukiwa wa 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen msimu wa 2000-01.
•Madrid inaweka rekodi ya kucheza Nusu Fainali ya 23 katika michuano hiyo mikubwa Ulaya na inatarajiwa kucheza Fainali ya 13.
•Cristiano Ronaldo ameifungia Real Hat Tricks 14 katika La Liga pekee, mbili zaidi dhidi ya Ferenc Puskas katika rekodi ya jumla ya klabu hiyo, lakini bado yuko nyumka ya rekodi ya Alfredo Di Stefano aliyefunga 22.
VIKOSI VYA LEO:
BAYERN MUNICH: Neuer, Lahm, Boateng, Badstuber, Alaba, Gustavo, Kroos, Robben, Muller, Ribery na Gomez.REAL MADRID: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Khedira, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo na Benzema.
MFALME WA MABAO ITALI ATUNGIKA DALUGA, KISA KIFO CHA MCHEZAJI MWENZAKE JUMAMOSI
![]() |
Di Natale |
NAHODHA wa Udinese ya Italia, Antonio Di Natale amesemja anaweza kustaafu mwishoni mwa msimu, kufuatia kifo cha mchezaji mwenzake wa zamani, Piermario Morosini akiichezea Livorno Jumamosi.
Kijana wa umri wa miaka 25, Morosini, ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka klabu hiyo ya Serie A, Udinese, alizimia na kufariki dunia baada ya kupata tatizo la moyo katika mechi ya Serie B huko Pescara.Jana, Di Natale alisema soka inachezwa sana Italia na kwa hilo; ''mwaka jana nilifikiria kustaafu. ... nitacheza hizo mechi sita za mwisho kwa Mario na kasha tutaona.''
Di Natale ana umri wa miaka 34. Mshambuliaji huyo wa Itali amekuwa mfungaji bora wa Serie A kwa misimu miwili iliyopita.
Kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa mabao yake 20, akizidiwa matatu tu na Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan.
MUAMBA AREJEA NYUMBANI
![]() |
Muamba katikati na viongozi wa Bolton pembeni yake |
KIUNGO wa England mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Muamba, ambaye nusura afe baada ya moyo wake kusimama ameruhusiwa kutoka hospitali ya London Chest na kurejea nyumbani.
Muamba amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya moyo mjini London. Kiungo huyo wa Bolton Wanderers ya Ligi Kuu, alianguka uwanjani wakati klabu hiyo ikicheza na Tottenham katika Robo Fainali ya Kombe la FA.Amekuwa akisaidiwa na daktari aliyempa huduma ya kwanza alipoanguka uwanjani. Muamba amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia kupata muda na familia yake huku akiwarudishia shukurani mashabiki na wenzake ambao waliungana naye wakati wote akiwa hospitalini.
Hapo Jumamosi shirikisho la soka Italia lilisimamisha mechi zote baada ya mchezaji wa klabu ya Livorno, Piermario Morosini, kuzirahi na baadaye kufariki dunia alipokuwa akichezea klabu yake.
LULU ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 17 GEREZANI JANA
![]() |
Lulu kulia, hapa akiwa ,marehemu Kanumba katika moja ya filamu walizocheza pamoja |
MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' jana Jumatatu alitimiza miaka 17 akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Lulu, ambaye anashikiliwa katika gereza hilo akishtakiwa kwa madai ya kumuua msanii wa filamu Steven Kanumba, Jumatano iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, lakini hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za mauaji.Kwa mujibu wa cheti cha kuzaliwa ambacho Mwanaspoti imekiona, inaonyesha kuwa Lulu alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aprili 16, mwaka 1995.
Hiyo ina maana kuwa jana Jumatatu, Lulu alisherehea siku yake ya kuzaliwa, ingawa hakuna uhakika kama �alikula keki� gerezani.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu amesajiliwa kwa majina ya Diana Elizabeth, huku jina la baba likiwa ni Michael Edward Kimemeta na mama akiitwa Lucresia Agustino Kalugila.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu alizaliwa Aprili 16, 1995, lakini alisajiliwa siku tatu baadaye, yaani Aprili 19, mwaka huo.
Lulu, ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano iliyopita na kutotakiwa kujibu chochote, alitoa maelezo yake Polisi Jumatatu ya wiki iliyopita ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba Aprili 7.
Lulu alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.
Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) alitoka Makao Makuu kusaidia kufanya mahojiano na binti huyo ambaye mtoa taarifa wetu anasema hakuwa tayari kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo, lakini alitumia takribani muda wa saa tatu kumlainisha Lulu.
GAZETI LA MWANASPOTI LEO
Monday, April 16, 2012
ARSENAL WAPIGWA NYUMBANI, WAPOLEEE
![]() |
Wachezaji wa Wigan |
![]() |
Bao la Arsenal |
![]() |
Wigan wakishangilia, mabeki wa Arsenal wakiwa wameduwaa |
MABAO ya mapema ya Franco di Santo na Jordi Gomez, yameiwezesha Wigan kujitoa kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kuvuna ushindi wa kwanza kihistoria mbele ya Arsenal usiku huu Uwanja wa Emirates.
Hadi mapumziko, tayari Arsenal ilikuwa imekwishalowa 2-1, mabao ya Wigan yakitiwa kimiani na Di Santo dakika ya saba na Gomez dakika ya nane.Mabao ya hayo ya haraka haraka ya Wigan yaliwachanganya Arsenal na iliwachukua dakika 12 kukombo moja, likitiwa kimiani na Thomas Vermaelen dakika ya 21.
Pamoja na kipigo hicho, The Gunners wanabaki nafasi ya tatu kwenye msimamowa Ligi Kuu, kwa pointi zao 64, baada ya kucheza mechi 34.
Ikiwa katika nafasi ya nne, Tottenham ndio timu inayoitia jakamoyo Arsenal katika kinyang’anyiro cha nafasi ya tatu, kwani imecheza mechi 33 na ina pointi 59.
Wigan sasa iko nafasi ya 16 na kujitoa kwenye eneo la hatari, baada ya kufikisha pointi 34 katika mechi 34, ambayo ni sawa na wastani wa pointi moja kila mechi iliyocheza.
QPR imeshuka hadi nafasi ya 17, ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 34, wakati Bolton inabaki nafasi ya 18 kwa pointi zake 29 kwenye mechi 32, Blackburn pia inabaki nafasi ya 19 kwa pointi zake 28 kwenye mechi 34, wakati Wolves inaendelea kuzibeba timu nyingine zote 19 katika ligi kwa pointi zake 23, kwenye mechi 34.
ROONEY, VAN PERSIE WACHONGANISHWA PFA, NANI ATAIBUKA KIDUME?
![]() |
Van Persie |
![]() |
Rooney na Wellbeck |
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie ni miongoni mwa wachezaji sita walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England, PFA katika Ligi Kuu msimu.
Nahodha huyo Arsenal amekuwa na msimu mzuri akifunga mabao ya kutosha, hadi sasa akiwa ametikisa nyavu mara 27 katika ligi na kutoa pasi za mabao 10 kwa wachezaji wenzake.Alex Oxlade-Chamberlain, wakati huo huo ameingizwa kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Mshindi wa tuzo hizo anatarajiwa kutajwa Jumapili.
Orodha ya wanaowania tuzo Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA: Robin van Persie (Arsenal), Wayne Rooney (Manchester United), Scott Parker (Tottenham), Sergio Aguero, Joe Hart, David Silva (wote Manchester City).
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka PFA: Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Gareth Bale, Kyle Walker (both Tottenham), Danny Welbeck (Manchester United), Sergio Aguero (Manchester City), Daniel Sturridge (Chelsea).
KOLO TOURE KUBEBA JUMLA KIFAA CHAKE JUNI 16
![]() |
Kolo na mkewe mtarajiwa |
BEKI wa Manchester City, Kolo Toure anatarajia kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa watoto wake wawili, Chimene Akassou Juni 16 na 17 nchini Ivory Coast, amesema mchezaji huyo katika taarifa yake bongostaz.blogspot.com leo.
Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja England tangu mwaka 2003, mwaka mmoja tu tangu mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ajiunge na Arsenal, akitokea klabu yake iliyomuinua nchini mwao, Asec Mimosas.Baada ya kufunga ndoa Mairie de Cocody mjini Abidjan, sherehe zitaendelea kanisani na msikitni, imesema taarifa hiyo.
Toure, mwenye umri wa miaka 31, ni muumini wa dini ya Kiislamu, wakati mkewe mtarajiwa ni Mkristo.
Ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa katika nyota wa Ivory Coast na amecheza Fainali tatu za Kombe la Mataifa ya Afrika na mbili za Kombe la Dunia.
Machi mwaka 2011 alikutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni na akatumikia adhabu ya kusimama kucheza soka kwa miezi sita.
Ni kaka wa Mwansoka Bora Afrika na mchezaji mwenzake katika timu ya taifa na klabu ya Manchester City, Yaya Toure, na kaka wa mshambuliaji wa zamani wa OGC Nice, Ibrahim Toure.
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alimuoa rasmi mama wa watoto wake watatu, Lalla mwaka jana mjini Monaco, Ufaransa.
MARADONA: HUYU PELE ANAANZA KUWA CHIZI SASA
![]() |
Maradona kushoto, Messi kulia enzi hizo akiwa kocha wa Argnetina |
KOCHA wa Al Wasl ya Dubai, Diego Maradona amemsuta gwiji wa soka Brazil, Pele akimuita mnafiki kwa kusema mshambuliaji wa Santos, Neymar ni bora kuliko nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Pele alisema Jumanne iliyopita kwamba Messi ni mchezaji babu kubwa, lakini akasema hamfikii nyota huyo wa Santos."Mungu wangu, huo ni upumbavu," alisema Maradona katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com. "Labda Neymar ni mchezaji bora wa dunia, lakini tu ukisema Messi ni kutoka dunia nyingine."
Wachezaji wote hao waliingia kwenye tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or Gala, Januari mwaka huu na Messi akashinda tuzo hiyo kama mchezaji bora wa 2011, wakati Neymar akaambulia tuzo ya Puskas, inayotokana na bao bora la mwaka.
RATIBA WIKI HII DUNIA NZIMA NA MUDA
![]() |
Mechi kubwa zaidi wiki hii ni Chelsea na Barcelona |
RATIBA | WIKI HII
(Katika kila Muda ulioandikwa hapa, ongeza saa moja. kwa mfano 18:00 maana yake saa 1:00, 21:45 maana yake saa 4:45).
15 April 2012 | ||||
Botswana 2011/12 | ||||
14:00 | Tafic | v | UF Santos | UB Stadium |
14:00 | Mogoditshane Fighters | v | Centre Chiefs | Francistown Stadium |
Mozambique 2012 | ||||
16:30 | Ferroviario Beira | v | Maxaquene | Estadio do Machava |
16 April 2012 | ||||
Angola 2012 | ||||
17:00 | Progresso | v | Santos | Provincial da Huila |
Barclays Premier League | ||||
21:00 | Arsenal | v | Wigan | Emirates Stadium |
French Ligue 1 | ||||
21:00 | Rennes | v | Nice | Route de Lorient |
Spanish Primera Liga | ||||
21:00 | Getafe | v | Sevilla | Coliseum Alfonso Perez |
17 April 2012 | ||||
Absa Premiership | ||||
19:30 | Kaizer Chiefs | v | Maritzburg Utd | Peter Mokaba Stadium |
UEFA Champions League | ||||
20:45 | Bayern Munich | v | Real Madrid | Allianz Arena |
18 April 2012 | ||||
Absa Premiership | ||||
19:30 | AmaZulu | v | Golden Arrows | Moses Mabhida Stadium |
19:30 | Bidvest Wits | v | Ajax Cape Town | Bidvest Stadium |
19:30 | Free State Stars | v | Black Leopards | Charles Mopeli Stadium |
19:30 | Jomo Cosmos | v | Bloem Celtic | Nelson Mandela Bay Stadium |
19:30 | Santos | v | SuperSport United | Athlone Stadium |
19:30 | Mamelodi Sundowns | v | Platinum Stars | Lucas Moripe Stadium |
20:00 | Moroka Swallows | v | Orlando Pirates | Volkswagen Dobsonville Stadium |
French Ligue 1 | ||||
18:30 | Marseille | v | Caen | Stade Velodrome |
18:30 | Toulouse | v | Lyon | Stadium Municipal |
National First Division | ||||
15:00 | United FC | v | Thanda Royal Zulu FC | De Beers Stadium |
Tanzania 2012 | ||||
19:00 | Ruvu Shooting | v | Moro United | PWANI |
19:00 | JKT Ruvu | v | Simba SC | DAR ES SALAAM |
19:00 | Polisi Dodoma | v | Coastal Union | DODOMA |
19:00 | Villa Squad | v | African Lyon | DAR ES SALAAM |
UEFA Champions League | ||||
20:45 | Chelsea | v | Barcelona | Stamford Bridge |
19 April 2012 | ||||
UEFA Europa League | ||||
21:05 | Atletico Madrid | v | Valencia | Vicente Calderon |
21:05 | Sporting | v | Athletic Bilbao | Estadio Jose Alvalade |
20 April 2012 | ||||
Angola 2012 | ||||
19:00 | Benfica Luanda | v | Kobuscorp | Nossa Senhora do Moute |
German Bundesliga | ||||
20:30 | Mainz | v | Wolfsburg | Bruchwegstadion |
National First Division | ||||
20:00 | Dynamos | v | Chippa United | Giyani Stadium |
Portuguese Liga | ||||
21:15 | Pacos Ferreira | v | Braga | Estadio da Mata Real |
Uganda Super League | ||||
16:30 | BIDCO | v | UTODA | Kakindu Stadium |
16:30 | KCC FC | v | Masaka LC | Lugogo Stadium |
16:30 | Police FC | v | Fire Masters | Namboole Stadium |
21 April 2012 | ||||
Absa Premiership | ||||
15:00 | Golden Arrows | v | Jomo Cosmos | Princess Magogo Stadium |
15:00 | Platinum Stars | v | Free State Stars | Royal Bafokeng Stadium |
18:00 | Maritzburg Utd | v | Mamelodi Sundowns | Nelson Mandela Bay Stadium |
20:15 | Orlando Pirates | v | Bidvest Wits | Orlando Stadium |
20:15 | SuperSport United | v | Ajax Cape Town | Peter Mokaba Stadium |
Angola 2012 | ||||
16:00 | Recreativo do Libolo | v | Recreativo da Caala | Municipal do Tafe |
16:30 | Onze Bravos | v | Nacional de Benguela | Mundunduleno |
16:30 | Sporting Cabinda | v | Progresso | Mundunduleno |
16:30 | Sagarada Esperanca | v | Academica do Soyo | Martires da Kanhara |
17:00 | Santos | v | 1 de Agosto | Jose Eduardo dos Santos |
17:00 | ASA | v | Interclube | Imomdeira |
Barclays Premier League | ||||
13:45 | Arsenal | v | Chelsea | Emirates Stadium |
16:00 | Aston Villa | v | Sunderland | Villa Park |
16:00 | Blackburn | v | Norwich | Ewood Park |
16:00 | Bolton | v | Swansea | Reebok Stadium |
16:00 | Fulham | v | Wigan | Craven Cottage |
16:00 | Newcastle | v | Stoke | Sports Direct Arena |
18:30 | QPR | v | Tottenham | Loftus Road Stadium |
Botswana 2011/12 | ||||
16:00 | Extension Gunners | v | Gabarone United | Lobatse Stadium |
16:00 | UF Santos | v | FC Satmos | Molepolole Sports |
16:00 | BDF XI | v | Nico United | SSKB |
16:00 | Tafic | v | Police XI | Francistown Stadium |
19:30 | Centre Chiefs | v | Miscellaneous | Molepolole Sports |
French Ligue 1 | ||||
19:00 | Brest | v | Rennes | Francis le Ble |
19:00 | Caen | v | St Etienne | Michel-d'Ornano |
19:00 | Dijon | v | Lille | Gaston Gerard |
19:00 | Evian TG | v | Toulouse | Parc des Sports |
19:00 | Montpellier | v | Valenciennes | La Mosson |
19:00 | Nice | v | Auxerre | Municipal du Ray |
21:00 | Bordeaux | v | Marseille | Chaban-Delmas |
German Bundesliga | ||||
15:30 | Cologne | v | VfB Stuttgart | Rhein Energie Stadion |
15:30 | Hertha Berlin | v | FC Kaiserslautern | Olympiastadion |
15:30 | Nurnberg | v | Hamburg | easyCredit Stadion |
15:30 | TSG Hoffenheim | v | Bayer Leverkusen | Rhein-Neckar Arena |
15:30 | Werder Bremen | v | Bayern Munich | Weserstadion |
18:30 | Borussia Dortmund | v | Borussia M'gladbach | Signal Iduna Park |
Ghana Premier League 2011/12 | ||||
16:30 | Mighty Jets | v | Asante Kotoko | ACCRA Stadium |
Italy Serie A | ||||
18:00 | Chievo | v | Udinese | Bentegodi |
20:45 | Napoli | v | Novara | San Paolo |
Kenyan Premier League | ||||
13:00 | KCB | v | Karuturi Sports | City |
15:00 | Oserian | v | Muhoroni Youth | Oserian |
15:00 | Mathare United | v | Western Stima | City |
15:00 | SonySugar | v | Rangers | Awendo |
15:00 | Ulinzi Stars | v | Gor Mahia | Afraha |
15:00 | AFC Leopards | v | Tusker | |
Mozambique 2012 | ||||
16:30 | Chingale de Tete | v | Liga Muculmana | Estadio do Ferroviario |
16:30 | Costa do Sol | v | Incomati | Estadio do Lichinga |
16:30 | Textil de Pungue | v | Ferroviario Nampula | Estadio do Maxaquene |
16:30 | Maxaquene | v | Desportivo Maputo | Estadio Machava |
16:30 | Vilankulo | v | Ferroviario Beira | Camp da Atletico Muculmano |
16:30 | Ferroviario Pemba | v | Chibuto | Estadio da Soalpo |
16:30 | Desportivo Maputo | v | HCB Songo | Estadio do Desportivo |
National First Division | ||||
15:00 | FC Cape Town | v | Carara Kicks | NNK Rugby Stadium |
15:00 | Black Aces | v | F.C A.K | Volkswagen Dobsonville Stadium |
15:00 | Vasco Da Gama | v | United FC | Parow Park |
Portuguese Liga | ||||
18:00 | Benfica | v | Maritimo | Estadio da Luz |
20:15 | Guimaraes | v | Uniao Leiria | Estadio D. Afonso Henriques |
22:15 | FC Porto | v | Beira Mar | Estadio do Dragao |
Spanish Primera Liga | ||||
18:00 | Mallorca | v | Real Zaragoza | ONO Estadi |
18:00 | Sporting Gijon | v | Rayo Vallecano | El Molinon |
20:00 | Barcelona | v | Real Madrid | Camp Nou |
22:00 | Sevilla | v | Levante | Estadio Ramon Sanchez Pizjuan |
Tanzania 2012 | ||||
15:30 | Azam FC | v | Mtibwa Sugar | DAR ES SALAAM |
15:30 | Kagera Sugar | v | Toto African | KAGERA |
Uganda Super League | ||||
15:00 | Express FC | v | Water FC | Wankulukuku Stadium |
15:00 | URA | v | Maroons | Lugazi Stadium |
Zimbabwe 2012 / 2013 | ||||
16:30 | Dynamos | v | Black Mambas | Barbourfields |
16:30 | CAPS United | v | Harare City | Colliery |
16:30 | Hardbody | v | Hwange | Fufaro |
16:30 | Blue Rangers | v | Chicken Inn | Lafarge |
16:30 | Platinum | v | Shabanie Mine | Morris Depot |
16:30 | Quelaton | v | Motor Action | Motor Action Sports Club |
16:30 | Buffaloes | v | Highlanders | Mucheke |
16:30 | Monomotapa | v | Gunners | Rufaro |
22 April 2012 | ||||
Absa Premiership | ||||
15:00 | Bloem Celtic | v | Moroka Swallows | Botshabelo Stadium |
15:00 | Santos | v | Kaizer Chiefs | Athlone Stadium |
15:00 | Black Leopards | v | AmaZulu | Giyani Stadium |
Angola 2012 | ||||
17:00 | Petro de Luanda | v | Atletico Do Namibe | Cidale |
Barclays Premier League | ||||
13:30 | Man Utd | v | Everton | Old Trafford |
17:00 | Liverpool | v | West Brom | Anfield |
17:00 | Wolverhampton | v | Man City | Molineux Stadium |
Botswana 2011/12 | ||||
16:00 | BMC | v | Mogoditshane Fighters | Lobatse Stadium |
16:00 | Township Rollers | v | Notwane | Molepolole Sports |
16:00 | Ecco City Greens | v | GNT FC | Francistown Stadium |
French Ligue 1 | ||||
17:00 | AC Ajaccio | v | AS Nancy | Francois-Coty |
17:00 | PSG | v | Sochaux | Parc des Princes |
21:15 | Lyon | v | Lorient | Municipal De Gerland |
German Bundesliga | ||||
15:30 | Augsburg | v | Schalke 04 | Impuls Arena |
17:30 | Hannover 96 | v | SC Freiburg | AWD-Arena |
Ghana Premier League 2011/12 | ||||
16:30 | Heart of Lions | v | Adunana Stars | Kpando |
16:30 | Bechem United | v | Liberty Professionals | Bechem |
16:30 | AshantiGold FC | v | Medeama SC | Len Clay |
16:30 | Wassaman United | v | Edubiase FC | Sekondi |
16:30 | Hearts of Oak | v | Dwarfs | ACCRA Stadium |
16:30 | Arsenals | v | WA All Stars | Golden City Park |
16:30 | Tema Youth | v | Berekum Chelsea | Tema Stadium |
Italy Serie A | ||||
12:30 | Fiorentina | v | Inter Milan | Artemio Franchi |
15:00 | Catania | v | Atalanta | Angelo Massimino |
15:00 | AC Milan | v | Bologna | San Siro |
15:00 | Parma | v | Cagliari | Ennio Tardini |
15:00 | Lazio | v | Lecce | Stadio Olimpico |
15:00 | Cesena | v | Palermo | Dino Manuzzi |
15:00 | Genoa | v | Siena | Luigi Ferraris |
20:45 | Juventus | v | Roma | Juventus Stadium |
Kenyan Premier League | ||||
15:00 | City Stars | v | Chemelil Sugar | Hope Centre |
16:00 | Sofapaka | v | Thika United | Nyayo |
National First Division | ||||
15:00 | African Warriors | v | Bay United | Charles Mopeli Stadium |
15:00 | Atlie FC | v | Witbank Spurs | Makhulong Stadium |
15:00 | Thanda Royal Zulu FC | v | Blackburn Rovers | Richards Bay Sports Stadium |
15:00 | University of Pretoria | v | Sivutsa Stars | ABSA Tuks Stadium |
Portuguese Liga | ||||
17:00 | Gil Vicente | v | Rio Ave | Estadio Cidade de Barcelos |
17:00 | Feirense | v | Vitoria Setubal | Estadio Algarve |
20:15 | Nacional | v | Sporting | Estadio da Madeira |
Spanish Primera Liga | ||||
12:00 | Granada | v | Getafe | Los Carmenes |
12:00 | Real Sociedad | v | Villarreal | Anoeta |
17:00 | Racing Santander | v | Athletic Bilbao | El Sardinero |
18:00 | Atletico Madrid | v | Espanyol | Vicente Calderon |
21:30 | Valencia | v | Real Betis | Mestalla |
Tanzania 2012 | ||||
15:30 | Yanga SC | v | Polisi Dodoma | DAR ES SALAAM |