Tuesday, April 17, 2012

Tuesday, April 17, 2012

MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA BAYERN NA REAL LEO

Robben wa Bayern
Ronaldo wa Real
WENYEJI Bayern Munich watawarejesha kwenye kikosi cha kwanza Philipp Lahm, Franck Ribery na Mario Gomez katika mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa leo dhidi ya Real Madrid, baada ya wachezaji hao kupumzishwa mwishoni mwa wiki timu yao ikitoka sare na Mainz.
Bastian Schweinsteiger amerejea baad aya kutumikia adhabu ya mechi moja, lakini Jupp Heynckes amesema jana kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba hana uhakika kama Nahodha huyo Msaidizi ataanza kwa sababu alikosa mazoezi ya kujiandaa na mechi hiyo.
Toni Kroos anaweza kuwapo, wakati Luiz Gustavo anaweza kucheza kama kiungo wa pili wa ulinzi.
Mabeki Daniel Van Buyten anayeumwa mguu na Breno (goti) wote watakuwa nje.
Kocha wa Madrid, Jose Mourinho anatarajiwa kuwaanzisha pamoja Karim Benzema na Angel Di Maria baada ya wawili hao kukaa benchi Jumamosi timu yake ikishinda dhidi ya Sporting Gijon.
Xabi Alonso amerejea baada ya kumaliza adhabu, lakini Ricardo Carvalho na Lassana Diarra wote bado majeruhi na hawatacheza.

JE WAJUA?
•Bayern Munich imeshinda mechi sikta mfululizo za Ligi ya Mabingwa nyumbani na imeshinda mechi 12 kati ya 13 za Ulaya Allianz Arena.
•The Bavarian haijawahi kufungwa na na Real Madrid nyumbani (imeshinda nane na kutoa sare moja). Rekodi ya jumla ya Munich dhidi ya Madrid ni kushinda mechi 10, sare 2, kufungwa 6.
•Klabu hizo awali zimekutana katika Nusu Fainali nne, huku Bayern ikishinda mara tatu (1976, 1987 na 2001) na Madrid moja tu mwaka 2000.
•Jupp Heynckes, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa mchezaji wakiitoa Madrid msimu wa 1997-98, hajawahi kuifunga timu ya Hispania katika mechin mbili tangu awe kocha.
•Rekodi ya Real Madrid kutofungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu na ikiwa imefungwa mabao sita tu, inawafanya wawe timu yenye ukuta bora zaidi katika timu zote zilizosalia kwenye michuano hii.
•The Castilian wameshinda mechi moja tu katika ardhi ya Ujerumani katika mechi 22 (Kushinda 1, sare6, kufungwa 15) – ushindi pekee ukiwa wa 3-2 dhidi ya Bayer Leverkusen msimu wa 2000-01.
•Madrid inaweka rekodi ya kucheza Nusu Fainali ya 23 katika michuano hiyo mikubwa Ulaya na inatarajiwa kucheza Fainali ya 13.
•Cristiano Ronaldo ameifungia Real Hat Tricks 14 katika La Liga pekee, mbili zaidi dhidi ya Ferenc Puskas katika rekodi ya jumla ya klabu hiyo, lakini bado yuko nyumka ya rekodi ya Alfredo Di Stefano aliyefunga 22.

VIKOSI VYA LEO:
BAYERN MUNICH: Neuer, Lahm, Boateng, Badstuber, Alaba, Gustavo, Kroos, Robben, Muller, Ribery na Gomez.
REAL MADRID: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Khedira, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo na Benzema.

MFALME WA MABAO ITALI ATUNGIKA DALUGA, KISA KIFO CHA MCHEZAJI MWENZAKE JUMAMOSI

Di Natale
NAHODHA wa Udinese ya Italia, Antonio Di Natale amesemja anaweza kustaafu mwishoni mwa msimu, kufuatia kifo cha mchezaji mwenzake wa zamani, Piermario Morosini akiichezea Livorno Jumamosi.
Kijana wa umri wa miaka 25, Morosini, ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo kutoka klabu hiyo ya Serie A, Udinese, alizimia na kufariki dunia baada ya kupata tatizo la moyo katika mechi ya Serie B huko Pescara.
Jana, Di Natale alisema soka inachezwa sana Italia na kwa hilo; ''mwaka jana nilifikiria kustaafu. ... nitacheza hizo mechi sita za mwisho kwa Mario na kasha tutaona.''
Di Natale ana umri wa miaka 34. Mshambuliaji huyo wa Itali amekuwa mfungaji bora wa Serie A kwa misimu  miwili iliyopita.
Kwa sasa anashika nafasi ya pili kwa mabao yake 20, akizidiwa matatu tu na Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan.

MUAMBA AREJEA NYUMBANI

Muamba katikati na viongozi wa Bolton pembeni yake
KIUNGO wa England mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Muamba, ambaye nusura afe baada ya moyo wake kusimama ameruhusiwa kutoka hospitali ya London Chest na kurejea nyumbani.
Muamba amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya moyo mjini London. Kiungo huyo wa Bolton Wanderers ya Ligi Kuu, alianguka uwanjani wakati klabu hiyo ikicheza na Tottenham katika Robo Fainali ya Kombe la FA.
Amekuwa akisaidiwa na daktari aliyempa huduma ya kwanza alipoanguka uwanjani. Muamba amewaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia kupata muda na familia yake huku akiwarudishia shukurani mashabiki na wenzake ambao waliungana naye wakati wote akiwa hospitalini.
Hapo Jumamosi shirikisho la soka Italia lilisimamisha mechi zote baada ya mchezaji wa klabu ya Livorno, Piermario Morosini, kuzirahi na baadaye kufariki dunia alipokuwa akichezea klabu yake.

LULU ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 17 GEREZANI JANA

Lulu kulia, hapa akiwa ,marehemu Kanumba katika moja ya filamu walizocheza pamoja
MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' jana Jumatatu alitimiza miaka 17 akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Lulu, ambaye anashikiliwa katika gereza hilo akishtakiwa kwa madai ya kumuua msanii wa filamu Steven Kanumba, Jumatano iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, lakini hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa cheti cha kuzaliwa ambacho Mwanaspoti imekiona, inaonyesha kuwa Lulu alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aprili 16, mwaka 1995.
Hiyo ina maana kuwa jana Jumatatu, Lulu alisherehea siku yake ya kuzaliwa, ingawa hakuna uhakika kama alikula keki gerezani.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu amesajiliwa kwa majina ya Diana Elizabeth, huku jina la baba likiwa ni Michael Edward Kimemeta na mama akiitwa Lucresia Agustino Kalugila.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu alizaliwa Aprili 16, 1995, lakini alisajiliwa siku tatu baadaye, yaani Aprili 19, mwaka huo.
Lulu, ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano iliyopita na kutotakiwa kujibu chochote, alitoa maelezo yake Polisi Jumatatu ya wiki iliyopita ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba Aprili 7.
Lulu alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.
Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) alitoka Makao Makuu kusaidia kufanya mahojiano na binti huyo ambaye mtoa taarifa wetu anasema hakuwa tayari kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo, lakini alitumia takribani muda wa saa tatu kumlainisha Lulu.

GAZETI LA MWANASPOTI LEO

Monday, April 16, 2012

ARSENAL WAPIGWA NYUMBANI, WAPOLEEE


Wachezaji wa Wigan
Bao la Arsenal
Wigan wakishangilia, mabeki wa Arsenal wakiwa wameduwaa
MABAO ya mapema ya Franco di Santo na Jordi Gomez, yameiwezesha Wigan kujitoa kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kuvuna ushindi wa kwanza kihistoria mbele ya Arsenal usiku huu Uwanja wa Emirates.
Hadi mapumziko, tayari Arsenal ilikuwa imekwishalowa 2-1, mabao ya Wigan yakitiwa kimiani na Di Santo dakika ya saba na Gomez dakika ya nane.
Mabao ya hayo ya haraka haraka ya Wigan yaliwachanganya Arsenal na iliwachukua dakika 12 kukombo moja, likitiwa kimiani na Thomas Vermaelen dakika ya 21.
Pamoja na kipigo hicho, The Gunners wanabaki nafasi ya tatu kwenye msimamowa Ligi Kuu, kwa pointi zao 64, baada ya kucheza mechi 34.
Ikiwa katika nafasi ya nne, Tottenham ndio timu inayoitia jakamoyo Arsenal katika kinyang’anyiro cha nafasi ya tatu, kwani imecheza mechi 33 na ina pointi 59.
Wigan sasa iko nafasi ya 16 na kujitoa kwenye eneo la hatari, baada ya kufikisha pointi 34 katika mechi 34, ambayo ni sawa na wastani wa pointi moja kila mechi iliyocheza.
QPR imeshuka hadi nafasi ya 17, ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 34, wakati Bolton inabaki nafasi ya 18 kwa pointi zake 29 kwenye mechi 32, Blackburn pia inabaki nafasi ya 19 kwa pointi zake 28 kwenye mechi 34, wakati  Wolves inaendelea kuzibeba timu nyingine zote 19 katika ligi kwa pointi zake 23, kwenye mechi 34.

ROONEY, VAN PERSIE WACHONGANISHWA PFA, NANI ATAIBUKA KIDUME?

Van Persie
Rooney na Wellbeck
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie ni miongoni mwa wachezaji sita walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England, PFA katika Ligi Kuu msimu.
Nahodha huyo Arsenal amekuwa na msimu mzuri akifunga mabao ya kutosha, hadi sasa akiwa ametikisa nyavu mara 27 katika ligi na kutoa pasi za mabao 10 kwa wachezaji wenzake.
Alex Oxlade-Chamberlain, wakati huo huo ameingizwa kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Mshindi wa tuzo hizo anatarajiwa kutajwa Jumapili.
Orodha ya wanaowania tuzo Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA: Robin van Persie (Arsenal), Wayne Rooney (Manchester United), Scott Parker (Tottenham), Sergio Aguero, Joe Hart, David Silva (wote Manchester City).
Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka PFA: Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Gareth Bale, Kyle Walker (both Tottenham), Danny Welbeck (Manchester United), Sergio Aguero (Manchester City), Daniel Sturridge (Chelsea).

KOLO TOURE KUBEBA JUMLA KIFAA CHAKE JUNI 16

Kolo na mkewe mtarajiwa
BEKI wa Manchester City, Kolo Toure anatarajia kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi na mama wa watoto wake wawili, Chimene Akassou Juni 16 na 17 nchini Ivory Coast, amesema mchezaji huyo katika taarifa yake bongostaz.blogspot.com leo.
Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja England tangu mwaka 2003, mwaka mmoja tu tangu mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ajiunge na Arsenal, akitokea klabu yake iliyomuinua nchini mwao, Asec Mimosas.
Baada ya kufunga ndoa Mairie de Cocody mjini Abidjan, sherehe zitaendelea kanisani na msikitni, imesema taarifa hiyo.
Toure, mwenye umri wa miaka 31, ni muumini wa dini ya Kiislamu, wakati mkewe mtarajiwa ni Mkristo.
Ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa katika nyota wa Ivory Coast na amecheza Fainali tatu za Kombe la Mataifa ya Afrika na mbili za Kombe la Dunia.
Machi mwaka 2011 alikutwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni na akatumikia adhabu ya kusimama kucheza soka kwa miezi sita.
Ni kaka wa Mwansoka Bora Afrika na mchezaji mwenzake katika timu ya taifa na klabu ya Manchester City, Yaya Toure, na kaka wa mshambuliaji wa zamani wa OGC Nice, Ibrahim Toure.
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba alimuoa rasmi mama wa watoto wake watatu, Lalla mwaka jana mjini Monaco, Ufaransa.

MARADONA: HUYU PELE ANAANZA KUWA CHIZI SASA

Maradona kushoto, Messi kulia enzi hizo akiwa kocha wa Argnetina
KOCHA wa Al Wasl ya Dubai, Diego Maradona amemsuta gwiji wa soka Brazil, Pele akimuita mnafiki kwa kusema mshambuliaji wa Santos, Neymar ni bora kuliko nyota wa Barcelona, Lionel Messi.
Pele alisema Jumanne iliyopita kwamba Messi ni mchezaji babu kubwa, lakini akasema hamfikii nyota huyo wa Santos.
"Mungu wangu, huo ni upumbavu," alisema Maradona katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com. "Labda Neymar ni mchezaji bora wa dunia, lakini tu ukisema Messi ni kutoka dunia nyingine."
Wachezaji wote hao waliingia kwenye tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or Gala, Januari mwaka huu na Messi akashinda tuzo hiyo kama mchezaji bora wa 2011, wakati Neymar akaambulia tuzo ya Puskas, inayotokana na bao bora la mwaka.

RATIBA WIKI HII DUNIA NZIMA NA MUDA

Mechi kubwa zaidi wiki hii ni Chelsea na Barcelona

RATIBA | WIKI HII

(Katika kila Muda ulioandikwa hapa, ongeza saa moja. kwa mfano 18:00 maana yake saa 1:00, 21:45 maana yake saa 4:45). 
15 April 2012
Botswana 2011/12
14:00 Tafic v UF Santos UB Stadium
14:00 Mogoditshane Fighters v Centre Chiefs Francistown Stadium
Mozambique 2012
16:30 Ferroviario Beira v Maxaquene Estadio do Machava
16 April 2012
Angola 2012
17:00 Progresso v Santos Provincial da Huila
Barclays Premier League
21:00 Arsenal v Wigan Emirates Stadium
French Ligue 1
21:00 Rennes v Nice Route de Lorient
Spanish Primera Liga
21:00 Getafe v Sevilla Coliseum Alfonso Perez
17 April 2012
Absa Premiership
19:30 Kaizer Chiefs v Maritzburg Utd Peter Mokaba Stadium
UEFA Champions League
20:45 Bayern Munich v Real Madrid Allianz Arena
18 April 2012
Absa Premiership
19:30 AmaZulu v Golden Arrows Moses Mabhida Stadium
19:30 Bidvest Wits v Ajax Cape Town Bidvest Stadium
19:30 Free State Stars v Black Leopards Charles Mopeli Stadium
19:30 Jomo Cosmos v Bloem Celtic Nelson Mandela Bay Stadium
19:30 Santos v SuperSport United Athlone Stadium
19:30 Mamelodi Sundowns v Platinum Stars Lucas Moripe Stadium
20:00 Moroka Swallows v Orlando Pirates Volkswagen Dobsonville Stadium
French Ligue 1
18:30 Marseille v Caen Stade Velodrome
18:30 Toulouse v Lyon Stadium Municipal
National First Division
15:00 United FC v Thanda Royal Zulu FC De Beers Stadium
Tanzania 2012
19:00 Ruvu Shooting v Moro United PWANI
19:00 JKT Ruvu v Simba SC DAR ES SALAAM
19:00 Polisi Dodoma v Coastal Union DODOMA
19:00 Villa Squad v African Lyon DAR ES SALAAM
UEFA Champions League
20:45 Chelsea v Barcelona Stamford Bridge
19 April 2012
UEFA Europa League
21:05 Atletico Madrid v Valencia Vicente Calderon
21:05 Sporting v Athletic Bilbao Estadio Jose Alvalade
20 April 2012
Angola 2012
19:00 Benfica Luanda v Kobuscorp Nossa Senhora do Moute
German Bundesliga
20:30 Mainz v Wolfsburg Bruchwegstadion
National First Division
20:00 Dynamos v Chippa United Giyani Stadium
Portuguese Liga
21:15 Pacos Ferreira v Braga Estadio da Mata Real
Uganda Super League
16:30 BIDCO v UTODA Kakindu Stadium
16:30 KCC FC v Masaka LC Lugogo Stadium
16:30 Police FC v Fire Masters Namboole Stadium
21 April 2012
Absa Premiership
15:00 Golden Arrows v Jomo Cosmos Princess Magogo Stadium
15:00 Platinum Stars v Free State Stars Royal Bafokeng Stadium
18:00 Maritzburg Utd v Mamelodi Sundowns Nelson Mandela Bay Stadium
20:15 Orlando Pirates v Bidvest Wits Orlando Stadium
20:15 SuperSport United v Ajax Cape Town Peter Mokaba Stadium
Angola 2012
16:00 Recreativo do Libolo v Recreativo da Caala Municipal do Tafe
16:30 Onze Bravos v Nacional de Benguela Mundunduleno
16:30 Sporting Cabinda v Progresso Mundunduleno
16:30 Sagarada Esperanca v Academica do Soyo Martires da Kanhara
17:00 Santos v 1 de Agosto Jose Eduardo dos Santos
17:00 ASA v Interclube Imomdeira
Barclays Premier League
13:45 Arsenal v Chelsea Emirates Stadium
16:00 Aston Villa v Sunderland Villa Park
16:00 Blackburn v Norwich Ewood Park
16:00 Bolton v Swansea Reebok Stadium
16:00 Fulham v Wigan Craven Cottage
16:00 Newcastle v Stoke Sports Direct Arena
18:30 QPR v Tottenham Loftus Road Stadium
Botswana 2011/12
16:00 Extension Gunners v Gabarone United Lobatse Stadium
16:00 UF Santos v FC Satmos Molepolole Sports
16:00 BDF XI v Nico United SSKB
16:00 Tafic v Police XI Francistown Stadium
19:30 Centre Chiefs v Miscellaneous Molepolole Sports
French Ligue 1
19:00 Brest v Rennes Francis le Ble
19:00 Caen v St Etienne Michel-d'Ornano
19:00 Dijon v Lille Gaston Gerard
19:00 Evian TG v Toulouse Parc des Sports
19:00 Montpellier v Valenciennes La Mosson
19:00 Nice v Auxerre Municipal du Ray
21:00 Bordeaux v Marseille Chaban-Delmas
German Bundesliga
15:30 Cologne v VfB Stuttgart Rhein Energie Stadion
15:30 Hertha Berlin v FC Kaiserslautern Olympiastadion
15:30 Nurnberg v Hamburg easyCredit Stadion
15:30 TSG Hoffenheim v Bayer Leverkusen Rhein-Neckar Arena
15:30 Werder Bremen v Bayern Munich Weserstadion
18:30 Borussia Dortmund v Borussia M'gladbach Signal Iduna Park
Ghana Premier League 2011/12
16:30 Mighty Jets v Asante Kotoko ACCRA Stadium
Italy Serie A
18:00 Chievo v Udinese Bentegodi
20:45 Napoli v Novara San Paolo
Kenyan Premier League
13:00 KCB v Karuturi Sports City
15:00 Oserian v Muhoroni Youth Oserian
15:00 Mathare United v Western Stima City
15:00 SonySugar v Rangers Awendo
15:00 Ulinzi Stars v Gor Mahia Afraha
15:00 AFC Leopards v Tusker
Mozambique 2012
16:30 Chingale de Tete v Liga Muculmana Estadio do Ferroviario
16:30 Costa do Sol v Incomati Estadio do Lichinga
16:30 Textil de Pungue v Ferroviario Nampula Estadio do Maxaquene
16:30 Maxaquene v Desportivo Maputo Estadio Machava
16:30 Vilankulo v Ferroviario Beira Camp da Atletico Muculmano
16:30 Ferroviario Pemba v Chibuto Estadio da Soalpo
16:30 Desportivo Maputo v HCB Songo Estadio do Desportivo
National First Division
15:00 FC Cape Town v Carara Kicks NNK Rugby Stadium
15:00 Black Aces v F.C A.K Volkswagen Dobsonville Stadium
15:00 Vasco Da Gama v United FC Parow Park
Portuguese Liga
18:00 Benfica v Maritimo Estadio da Luz
20:15 Guimaraes v Uniao Leiria Estadio D. Afonso Henriques
22:15 FC Porto v Beira Mar Estadio do Dragao
Spanish Primera Liga
18:00 Mallorca v Real Zaragoza ONO Estadi
18:00 Sporting Gijon v Rayo Vallecano El Molinon
20:00 Barcelona v Real Madrid Camp Nou
22:00 Sevilla v Levante Estadio Ramon Sanchez Pizjuan
Tanzania 2012
15:30 Azam FC v Mtibwa Sugar DAR ES SALAAM
15:30 Kagera Sugar v Toto African KAGERA
Uganda Super League
15:00 Express FC v Water FC Wankulukuku Stadium
15:00 URA v Maroons Lugazi Stadium
Zimbabwe 2012 / 2013
16:30 Dynamos v Black Mambas Barbourfields
16:30 CAPS United v Harare City Colliery
16:30 Hardbody v Hwange Fufaro
16:30 Blue Rangers v Chicken Inn Lafarge
16:30 Platinum v Shabanie Mine Morris Depot
16:30 Quelaton v Motor Action Motor Action Sports Club
16:30 Buffaloes v Highlanders Mucheke
16:30 Monomotapa v Gunners Rufaro
22 April 2012
Absa Premiership
15:00 Bloem Celtic v Moroka Swallows Botshabelo Stadium
15:00 Santos v Kaizer Chiefs Athlone Stadium
15:00 Black Leopards v AmaZulu Giyani Stadium
Angola 2012
17:00 Petro de Luanda v Atletico Do Namibe Cidale
Barclays Premier League
13:30 Man Utd v Everton Old Trafford
17:00 Liverpool v West Brom Anfield
17:00 Wolverhampton v Man City Molineux Stadium
Botswana 2011/12
16:00 BMC v Mogoditshane Fighters Lobatse Stadium
16:00 Township Rollers v Notwane Molepolole Sports
16:00 Ecco City Greens v GNT FC Francistown Stadium
French Ligue 1
17:00 AC Ajaccio v AS Nancy Francois-Coty
17:00 PSG v Sochaux Parc des Princes
21:15 Lyon v Lorient Municipal De Gerland
German Bundesliga
15:30 Augsburg v Schalke 04 Impuls Arena
17:30 Hannover 96 v SC Freiburg AWD-Arena
Ghana Premier League 2011/12
16:30 Heart of Lions v Adunana Stars Kpando
16:30 Bechem United v Liberty Professionals Bechem
16:30 AshantiGold FC v Medeama SC Len Clay
16:30 Wassaman United v Edubiase FC Sekondi
16:30 Hearts of Oak v Dwarfs ACCRA Stadium
16:30 Arsenals v WA All Stars Golden City Park
16:30 Tema Youth v Berekum Chelsea Tema Stadium
Italy Serie A
12:30 Fiorentina v Inter Milan Artemio Franchi
15:00 Catania v Atalanta Angelo Massimino
15:00 AC Milan v Bologna San Siro
15:00 Parma v Cagliari Ennio Tardini
15:00 Lazio v Lecce Stadio Olimpico
15:00 Cesena v Palermo Dino Manuzzi
15:00 Genoa v Siena Luigi Ferraris
20:45 Juventus v Roma Juventus Stadium
Kenyan Premier League
15:00 City Stars v Chemelil Sugar Hope Centre
16:00 Sofapaka v Thika United Nyayo
National First Division
15:00 African Warriors v Bay United Charles Mopeli Stadium
15:00 Atlie FC v Witbank Spurs Makhulong Stadium
15:00 Thanda Royal Zulu FC v Blackburn Rovers Richards Bay Sports Stadium
15:00 University of Pretoria v Sivutsa Stars ABSA Tuks Stadium
Portuguese Liga
17:00 Gil Vicente v Rio Ave Estadio Cidade de Barcelos
17:00 Feirense v Vitoria Setubal Estadio Algarve
20:15 Nacional v Sporting Estadio da Madeira
Spanish Primera Liga
12:00 Granada v Getafe Los Carmenes
12:00 Real Sociedad v Villarreal Anoeta
17:00 Racing Santander v Athletic Bilbao El Sardinero
18:00 Atletico Madrid v Espanyol Vicente Calderon
21:30 Valencia v Real Betis Mestalla
Tanzania 2012
15:30 Yanga SC v Polisi Dodoma DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment